Taiwan imesema uchumi wake ulikua kwa asilimia 8.63 ukiondoa mfumuko wa bei mwaka 2025, kutoka mwaka uliotangulia, ikiwa ni ukuaji wake wa juu zaidi katika kipindi cha miaka 15. Sababu kuu ilikuwa ni ongezeko kubwa la mauzo ya nje ya sakiti changamano na bidhaa zingine, yakichochewa na matumizi yanayoongezeka ya akili unde.

Baraza la Mawaziri la Taiwan, lilitoa data za awali za pato ghafi la ndani Januari 30. Mnamo mwaka 2010, uchumi ulizidi asilimia 10 baada ya kurejea katika hali yake ya kawaida kutoka kwenye mdororo wa kifedha duniani.

Mauzo ya nje ya sakiti changamano yaliongezeka kadiri matumizi ya akili unde yalivyoongezeka. Hasa, jumla ya mauzo ya nje kwenda Marekani yalifikia kiwango cha juu zaidi, yakizidi yale ya kwenda China.

Matumizi ya kibinafsi pia yalikuwa na nguvu na yalichangia ukuaji thabiti.

Mtaalamu wa uhasibu na takwimu wa baraza la mawaziri, Chiang Hsin-yi, alisema mahitaji ya sakiti changamano yalikuwa makubwa kuliko ilivyotarajiwa na yanaendelea kukua. Chiang alisema Marekani haijaweka viwango vya juu vya ushuru wa forodha kwa Taiwan na maagizo ya ununuzi yamekuwa imara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *