
Serikali ya mkoa wa Tshopo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imeliishutumu kundi la waasi la AFC/M23 linaloungwa mkono na Rwanda kwa kushambulia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bangboka, ulioko kilomita 17 kutoka katikati mwa jiji la Kisangani. Kulingana na mamlaka za mkoa huo, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yalifanyika kati ya saa 11:00 asubuhi siku ya Jumamosi, Januari 31, na saa 8:00 usiku siku ya Jumapili, Februari 1. Mamlaka za mkoa huo zinatoa wito wa utulivu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashambulizi haya ya ndege zisizo na rubani, yaliyotokea kati ya Jumamosi na Jumapili, yalisababisha mvutano mkubwa membezoni mwa uwanja wa ndege kabla ya kuzuiwa na jeshi la Kongo (FARDC) na washirika wake. Serikali ya mkoa wa Tshopo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inawahakikishia wakazi wa Kisangani na mkoa mzima wa Tshopo kwamba hali imedhibitiwa kabisa. Vikosi vya ulinzi na usalama vinatoa wito wa utulivu.
Hali imedhibitiwa, kulingana na mamlaka za mkoa. Senold Tandia Akomboyo, waziri wa mkoa na msemaji wa serikali ya Tshopo, anawasihi wakazi kurudi nyumbani, kwani hali imedhibitiwa: “Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bangboka ulilengwa na shambulio lililotekelezwa na ndege zisizo na rubani. Ndege nane zisizo na rubani za adui ziliharibiwa, na hakuna hata moja iliyoweza kufikia lengo lake iliyokusudia,” alisema. “Serikali ya mkoa wa Tshopo inalaani jaribio hili la kigaidi kwa nguvu zote na inavipongeza kwa dhati Vikosi vya Jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) kwa kujitolea kwao kusikotetereka kulinda uadilifu wa eneo letu.” Ukiukaji huu dhahiri wa sheria za kimataifa unaonyesha, tena, nia ya Rwanda ya kudhoofisha makubaliano ya amani yaliyosainiwa Washington, kinyume kabisa na ahadi zake. Walipowasiliana na RFI, M23 walikataa kutoa maoni yao.