Mkoa wa Aomori ulioko kaskazini mashariki mwa Japani umeomba Kikosi cha Kujihami cha Ardhini cha Japani, GSDF, kutuma maafisa katika mji wa Aomori ili kukabiliana na theluji nyingi iliyovunja rekodi.

Ombi hilo lililowasilishwa na mkoa huo linajumuisha kukusanya taarifa katika mji wa Aomori. Pia unaiomba GSDF kuwasaidia wazee wanaoishi peke yao kuondoa theluji kutoka kwenye paa zao.

Mwezi uliopita, mkoa huo uliamua kutumia sheria ya usaidizi wakati wa majanga kwa manispaa zake 15, ikiwa ni pamoja na mji wa Aomori, ili kufidia kiasi cha gharama ya kuondoa theluji kwa wale wasio na uwezo wa kufanya hivyo peke yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *