Mikoa ya kaskazini mwa Japani imekabiliwa na theluji nyingi zaidi kuliko kawaida. Theluji bado inadondoka katika maeneo ya pwani kando ya Bahari ya Japani.

Maeneo hayo yamekabiliwa na theluji iliyozidi wastani tangu baridi kali lilipoanza mwezi uliopita.

Kufikia saa 11 alfajiri Februari 3, jiji la Aomori lilikuwa na takriban theluji ya mita 1.75 ardhini, zaidi ya mara mbili ya wastani kwa wakati huu wa mwaka. Na katika jiji la Shinjo, mkoa wa Yamagata theluji ya mita 1.64 ilituama ardhini; mita 1.37 katika jiji la Kazuno, mkoa wa Akita; mita 1.35 katika jiji la Nagaoka, mkoa wa Niigata; na mita moja huko Sapporo.

Hewa ya majira ya baridi kali inatarajiwa kuanza kupungua polepole kutoka magharibi Februari 3. Watu wanashauriwa kuwa waangalifu kuhusu maporomoko ya theluji na theluji inayoanguka kutoka kwenye paa. Mamlaka inaonya kwamba kukatika kwa umeme kunawezekana, kwani theluji imekusanyika kwenye nyaya za umeme na miti iliyo karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *