.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Rais wa
zamani wa Marekani Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Nje, wamekubali kutoa ushahidi Bungeni katika uchunguzi unaoendelea wa
mhalifu wa kingono marehemu Jeffrey Epstein.

Naibu mkuu
wa wafanyakazi wa Bill Clinton alithibitisha habari hizo kwenye mitandao ya
kijamii, akiandika: “Rais wa zamani na Katibu wa zamani wa Mambo ya Nje
watafika” bungeni.

Hii inakuja
wakati Bunge la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na chama cha Republican linapojitayarisha
kupiga kura juu ya Rais huyo wa zamani na mkewe kuonyesha kudharau kwa kupuuza
wito wa kisheria.

Picha ya
Bill Clinton inaonekana katika faili za Epstein zilizotolewa na Idara ya
Sheria, ingawa rais huyo wa zamani wa chama cha Democratic amekanusha kufanya
makosa yoyote.

Haijulikani
wazi ni lini hilo litafanyika, lakini itakuwa mara ya kwanza kwa rais wa zamani
wa Marekani kutoa ushahidi kwa kamati ya bunge tangu Gerald Ford alipofanya
hivyo mwaka wa 1983.

Kamati ya
Uangalizi ya Bunge la Wawakilishi, ikiongozwa na Warepublican, iliidhinisha kupiga
kura juu ya rais huyo wa zamani na mkewe kwa kuonyesha dharau mwishoni mwa
mwezi uliopita, na kuungwa mkono na Wanademokrat kadhaa.

Katika
taarifa yake wakati huo, mwenyekiti wa kamati James Comer alisema “hakuna
mtu aliye juu ya sheria”.

Bill Clinton
hajawahi kushtakiwa kwa makosa yoyote na walionusurika na unyanyasaji wa
Epstein, na amekana kuhusika na kosa lake la unyanyasaji wa kijinsia.

Clinton na
mkewe pia wanasema kwamba hapo awali waliipa Kamati ya Uangalizi ya Bunge la
Wawakilishi taarifa za kiapo kama sehemu ya uchunguzi – na kwamba hawana ufahamu
wowote wenye kuhusiana na uchunguzi huo.

Bill Clinton
ameonekana na Epstein katika jengo la mhalifu huyo aliyefariki dunia kwenye picha
zilizotolewa na idara ya sheria baada ya Bunge kupitisha sheria inayoitaka Idara
hiyo kutoa nyenzo zinazohusiana na uchunguzi wa Epstein.

Picha moja
inaonyesha rais huyo wa zamani akiogelea kwenye bwawa la kuogelea, na nyingine
inamwonyesha amelala chali huku mikono yake ikiwa nyuma ya kichwa chake katika
kile kinachoonekana kama beseni la maji moto.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *