Utawala wa Marekani unatarajia kupokea takriban wawkilishi wa nchi zaidi ya arobaini mjini Washington leo Jumatano, Februari 4, 2026, kwa ajili ya mkutano kuhusu madini muhimu. Mkutano huo, ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, utajumuisha ujumbe wa Kongo kutoka Kinshasa, ambao uliwasili Washington ukiandamana na rais Félix Tshisekedi. Ujumbe mwingine kutoka Guinea na Kenya pia unatarajiwa kwa ajili ya mkutano huo.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya Washington, Rais wa Kongo Félix Tshisekedi amerejea katika mji mkuu wa Marekani, Washington, akiongoza ujumbe kushiriki katika mkutano kuhusu madini muhimu. Utawala wa Trump unatafuta kuimarisha usambazaji wake wa madini muhimu ili kukabiliana na utawala wa China, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasalia kuwa muhimu linapokuja suala la koltani, kobalti, na lithiamu, anasema mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi.

Wiki moja baada ya kuwakaribisha wenzake wa G7, Waziri  wa Fedha wa Marekani Scott Bessent anawaalika “washirika kutoka kote ulimwenguni” kujadili kupata rasilimali za kimkakati.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tayari imefikia makubaliano kuhusu madini na Washington, lakini hakuna miradi ambayo imekamilika. Uuzaji wa Chemaf unaendelea – mgodi huu wa shaba-kobalti ulioko Mutoshi kusini mwa nchi unakaribia kununuliwa na kampuni ya Marekani. Amana hii ilitolewa awali kwa wawekezaji wa China kabla ya Kinshasa kuingilia kati.

Wajumbe kutoka Guinea na Kenya pia kushiriki mkutano

Ujumbe wa Guinea pia utakuwepo Washington. Maslahi ya Conakry yapo katika kuunda uhusiano wa karibu na Marekani ili kuhimiza uwekezaji katika madini ya Bauxite na madini ya chuma, na hivyo kupunguza utegemezi wake kwa China, ambayo ina uwepo mkubwa katika sekta ya madini ya Guinea.

Nchi nyingine ya Afrika inayotarajiwa kuhudhuria ni Kenya, ambayo pia inaimarisha uhusiano wake na Marekani. Katikati ya matarajio ya Marekani ni akiba ya madini ya Mrima Hill kusini-mashariki mwa nchi, eneo lenye misitu linaloaminika kuwa na madini adimu ya ardhi yenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dola.

Kufuatia mwelekeo huu wa kiuchumi zaidi, Rais Tshisekedi amepangwa kushiriki katika Kiamsha kinywa cha Maombi ya Kitaifa ya 79 “National Prayer Breakfast”. Tukio hili la kila mwaka huwaleta pamoja watu mashuhuri ili kukuza sala na tafakari. Wabunge na rais wa Marekani wanatarajiwa kujiunga na rais wa Kongo.

Wageni wengine kutoka Kinshasa ni pamoja na kiongozi wa upinzani wa Kongo Martin Fayulu na viongozi wa kidini kutoka CENCO-ECC (Baraza la kitaifa la Maaskofu wa Kongo). Makanisa ya Katoliki na Kiprotestanti ya Kongo yamekuwa yakiongoza mpango kwa zaidi ya mwaka mmoja wa kuandaa mazungumzo kati ya Kongo ili kukomesha migogoro ya kisiasa na usalama nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *