Raia wanne wameuawa na pikipiki sita kuchomwa moto katika shambulio lililohusishwa na waasi wa ADF siku ya Jumanne, Februari 3, katika kijiji cha Mulolya, kilichopo kilomita kumi magharibi mwa wilaya ya vijijini ya Oicha, mji mkuu wa eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya usalama, shambulio hilo lilitokea yapata saa 2:00 asubuhi kwa saa za mashariki mwa DRC.

Waasi wa ADF, wakitokea magharibi mwa Mamove, eneo ambalo lilishambuliwa siku mbili mapema, walifanya shambulio la kuvizia dhid ya wasafiri kwenye barabara ya Oicha-Mulolya-Mamove.

Wasafiri wanne waliuawa na pikipiki sita kuchomwa moto kulingana na Radio OKAPI, ikinukuu mashahidi.

Shambulio hili linafikisha idadi ya raia waliouawa katika eneo hilo hadi tisa katika kipindi cha siku tatu tu.

Pia katika eneo hilo, lakini huko Malibo, shambulio lingine la aina hiyo liliripotiwa siku hiyo. Wakulima waliokuwa wamengwa walifanikiwa kutoroka na kuwasili Oicha.

Shuguli za usafiri zimisitishwa kwenye barabara hii, huku miili ya waathiriwa ikisafirishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Kuu ya Oicha na vijana wa kujitolea.

Tangu mashambulizi ya Jumapili, Februari 1, huko Mamove, Mbingi, na Vuhira, wilaya ya vijijini ya Oicha imekuwa ikiwapa hifadhi watu wengi waliohama makazi yao wakikimbia shughuli za waasi wa ADF.

Wakati huo huo, Naibu Mkuu wa jeshi anayesimamia shughuli za FARDC (Vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) yuko katika kazi ya kutathmini hali ya usalama huko Beni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *