
Watu wenye silaha wameua watu wasiopungua 35 katika kijiji cha Woro, katika Jimbo la Kwara, katikati-magharibi mwa Nigeria, kulingana na mbunge wa eneo hilo, katika shambulio lililothibitishwa na polisi na gavana wa jimbo la Kwara.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio jipya limegjharimu maisha ya watu wasiopungua 35 nchini Nigeria siku ya Jumanne, huku nchi hiyo ikiongeza juhudi zake za kupambana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na magenge ya wahalifu na wanajihadi, kwa usaidizi kutoka Marekani.
Jimbo la Kwara linakabiliwa na ukosefu wa usalama wa pande nyingi, ikiwa ni pamoja na magenge yenye silaha (wanaoitwa majambazi) ambao hupora vijiji, huteka nyara, na kuwatisha wakazi, na tishio linaloongezeka la wanajihadi, huku makundi yakiendelea kaskazini magharibi mwa nchi yakipanua shughuli zao kuelekea kusini.
Kutokana na ukosefu huu wa usalama, mamlaka za eneo hilo zimetangaza sheria ya kutotoka nje katika baadhi ya maeneo ya jimbo na kufunga shule kwa wiki kadhaa kabla ya kuagiza kufunguliwa tena siku ya Jumatatu.
“Asubuhi ya leo, niliambiwa kwamba miili 35 hadi 40 imehesabiwa, lakini sijaweza kuthibitisha hilo. Wengine wengi wamekimbilia msituni huku milio ya risasi ikisikika, na kuna uwezekano kwamba miili zaidi itapatikana msituni,” Sa’idu Baba Ahmed, mjumbe wa Bunge la Jimbo la Kwara, ameliambia shirika la habari la AFP.
Bw. Ahmed ameongeza kuwa majambazi hao walichoma moto maduka na jumba la kifalme la kijiji hicho. “Kwa sasa, hatujui mfalme yuko wapi,” alilalamika.
Polisi imethibitisha shambulio hilo lakini bado haijatoa hesabu ya majeruhi,na gavana wa Kwara amehusisha shambulio hilo na “makundi ya kigaidi.”