.

Chanzo cha picha, US Department of Justice via Press Association

Barua pepe
inayoonekana kutoka kwa Ghislaine Maxwell inaonekana kuthibitisha kwamba picha
ya Andrew Mountbatten-Windsor akiwa amemkumbatia Virginia Giuffre, ambaye
alimtuhumu kwa unyanyasaji wa kingono, ni ya ukweli.

Mwanamfalme
huyo wa zamani, ambaye amekuwa akikanusha kufanya makosa yoyote, hapo awali alisema
kuwa picha hiyo imefanyiwa ukarabati na kudai kuwa hajawahi kukutana na
Giuffre.

Lakini
katika ujumbe, uliotolewa kama sehemu ya kundi la hivi karibuni la faili za
Epstein, wenye kichwa “rasimu ya taarifa” iliyotumwa na “G
Maxwell” kwa Jeffrey Epstein mnamo mwaka 2015, aliandika: “Mnamo 2001
nilikuwa London wakati…nilikutana na marafiki zangu kadhaa akiwemo Prince
Andrew. Picha ilipigwa kwani nadhani alitaka kuionyesha kwa marafiki na
familia.”

Familia ya
Giuffre, ambaye alifariki mwaka wa 2025, iliambia kipindi cha Newsnight cha BBC
kwamba barua pepe hiyo ilionyesha kuwa alikuwa “akisema ukweli”.

“Kwa
kweli hii inamtetea Virginia… hakuwa akidanganya wakati huu wote”, kaka
yake Guiffre, Sky Roberts, alisema.

“Ni
wakati ambapo tunajivunia sana dada yetu,” aliongeza.

Barua pepe
hiyo, iliyotolewa na Idara ya Sheria ya Marekani (DoJ), inaongeza kwamba “G Maxwell” hakujua kuwa kuna “jambo lolote lisilofaa” linaloendelea
nyumbani kwake.

Jina la mtu
huyo limeondolewa kwenye toleo lililochapishwa la taarifa hiyo, lakini maelezo
yanaonyesha kwamba ni Maxwell aliyekuwa akimzungumzia Giuffre.

Giuffre –
mshtaki maarufu wa Epstein na Maxwell – inadaiwa kuwa Mountbatten-Windsor
alifanya naye mapenzi mara tatu akiwa kijana.

Daima
amekuwa akikanusha dai hilo na kufikia makubaliano ya nje ya mahakama na
Giuffre mwaka wa 2022. Hayakuwa na kukiri kuwajibika au kuomba msamaha.

BBC News
imewasiliana na wawakilishi wa Mountbatten-Windsor kwa ajili ya kutoa maoni
yao.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *