Serikali imekiri uwepo wa masharti magumu ya benki zinazotumika kutoa mikopo ya asilimia kumi na kufanya kuwa miongoni mwa sababu zinazokwamisha vikundi kupata huduma hiyo, jambo ambalo bado linaendelea kuzua malalamiko miongoni mwa wanufaika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Riziki Shemdoe amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Dodoma, Dkt. Neema Majule ambaye ametaka kufahamu ni lini serikali itaondoa mlolongo uliopo wa upatikanaji wa mikopo ya asilimia kumi hususan kwa wanawake wa vijijini.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *