Wananchi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha mkoani Lindi wametakiwa kujitokeza kwenye kambi ya upasuaji wa mabusha inayotarajiwa kutolewa na madaktari bingwa kuanzia Februari 9 – 25 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine.
Huduma hiyo inatarajiwa kutolewa bure, ambapo wananchi wamehimizwa kutumia fursa hiyo kupata matibabu ili waweze kuondokana na changamoto hiyo.
P#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi