s

Chanzo cha picha, AFP/East News/Radio Zet

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mazungumzo ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Iran yaliyofanyika Oman yamekamilika vyema na kwamba pande zote mbili zitaleta kikao kingine wiki ijayo, ingawa hakutoa maelezo zaidi kuhusu mkutano huo.

“Tulikuwa na kikao kizuri sana na mwakilishi wa juu kutoka Iran, na tutaona matokeo yatakavyokuwa,” Trump alisema mbele ya waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya Air Force One na kunukuliwa na NBC News. Aliongeza kuwa Iran haiwezi kuruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia chini ya makubaliano yoyote.

“Tutakutana tena mwanzoni mwa wiki ijayo, na Iran wanataka kufanya makubaliano, kama inavyopaswa. Wanajua matokeo kama wasipofanya makubaliano. Yatakuwa makubwa sana. Tutaona yanayofuatia,” Trump alisema.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, mazungumzo hayo hayakuwa ya ana kwa ana, bali pande zote ziliwasilisha msimamo wao kwa usimamizi wa Oman.

Mvutano kati ya Marekani na Iran umekuwa ukiongezeka, huku Trump akirudia kuonya kuhusu uwezekano wa shambulio la kijeshi. Vilevile, Marekani ilionyesha wazi uwezekano wa kuingilia kati kijeshi.

Kwa upande wa Iran, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi, alieleza kuwa mazungumzo hayo yalianza vyema. “Hii ilikuwa ni mwanzo mzuri. Hatua zinazofuata zitaamuliwa baada ya mashauriano ya ndani,” alisema kupitia ujumbe wa maandishi uliotumwa kwa vyombo vya habari ndani ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *