
Waziri wa Ulinzi wa DRC amesema wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri siku ya Ijumaa, Februari 6, kwamba vikosi vya jeshi la DRC (FARDC) vilizima mashambulizi ya “muungano wa RDF-M23-AFC” katika mkoa wa Kivu Kusini kwa kuchukuwa udhibiti wa maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na mjini kati Minembwe.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa sasa FARDC inaendelea na ulinzi wa eneo hilo katika nyanda za juu na za kati za Fizi, Uvira, na Mwenga, Waziri aliongeza.
Mnamo Februari 2, mamlaka ya kijeshi iliripoti kwamba FARDC ilisababisha hasara kubwa kwa muungano wa waasi katika eneo la Fizi, ikiwaangamaiza zaidi ya wapiganaji 30 wa M23/RDF na kuwakamata washirika wengine kadhaa, wakiwemo wapiganaji wa makundi ya Twigwaneho na Ngumino.
Licha ya mafanikio haya ya kijeshi, hali ya usalama bado ni dhaifu. Nyanda za Juu zinaendelea kushuhudia idadi kuwa ya wanajeshi, na raia wanaendelea kuteseka kutokana na mapigano, ikiwa ni pamoja na kuhama kwa raia wingi na vurugu.
Vyanzo vya misaada ya kibinadamu vinaripoti kwamba kuongezeka kwa mapigano ya silaha tangu mwezi Desemba 2025 huko Kivu Kusini kumesababisha zaidi ya watu 500,000 kuyahama makazi yao, hasa yakiathiri Uvira, Walungu, Mwenga, Shabunda, Kabare, Fizi na Kalehe.