Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa nishati wa Israel amesema kuwa makubaliano yanayoweza kufikiwa kati ya Washington na Tehran hayana maana yoyote.
“Hakuna thamani yoyote katika kufanya makubaliano na utawala wa sasa. Mabadiliko ya utawala mjini Tehran yako katika maslahi ya nchi zote za Kiislamu zinazoizunguka Iran,” Eli Cohen aliliambia chombo cha habari cha Israel, Ynet, siku ya Jumapili.
Bw. Cohen alisisitiza: “Hata kama makubaliano yatafikiwa, iwapo tishio litatokea dhidi ya Israel na tutalazimika kuchukua hatua, tutachukua hatua.”
Wawakilishi wa Iran na Marekani walifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Muscat siku ya Ijumaa, yakisimamiwa na Oman.
Muda na mahali pa mkutano unaofuata bado havijatangazwa.
Baraza la mawaziri la usalama la Israel, ambalo Eli Cohen ni mjumbe wake, linatarajiwa kukutana leo.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anasafiri kwenda Washington siku ya Jumatano kwa ajili ya kuzungumza na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mazungumzo na Iran.
Soma zaidi: