WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga wenye uwezo wa 2X60MVA 132/33kV, pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi.

Mradi huo unafadhiliwa na Serikali kwa gharama ya Sh bilioni 44.14 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme na Shs bilioni 5.75 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusambaza umeme.

Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya uimarishaji wa Gridi ya Taifa wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme katika wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika migodi ya Graphite katika Kijiji cha Kwamsisi.

Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *