Takriban watu 21 walikufa maji wakati boti iliyokuwa ikiwasafirisha ilipozama katika Mto Nile kaskazini mwa Sudan.

Jimbo la Mto Nile limearipoti kuwa miili 21 imepatikana baada ya ajali hiyo ya boti. Majina ya waliopoteza maisha yameorodheshwa na mamla husika zimetahadharisha kuwa baadhi ya abiria hadi sasa hawajapatikana. 

Boti iliyozama jana ilikuwa ikivuka mto kati ya vijiji vya Tayba al Khawad and Deim al Qarai. Hata hivyo chanzo cha ajali hakijatajwa. 

Watu walioshuhudia wamesema kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba watu 30 katika Mto Nile. Mtandao wa Madaktari wa Sudan umesema katika taarifa yake kuwa ni abiria sita tu ndio walionusurika na ajali hiyo ya kuzama boti. 

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeongeza kuwa ajali hiyo ya boti imeweka wazi kulegalega kwa usafiri wa mitoni na kukosekana kwa suhula muhimu za usalama pamoja na kutokuwepo kikamilifu kwa mamlaka husika na timu za ukoaji katika saa za mwanzo wakati ajali ilipotokea. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa Wasudani wengi wanategemea usafiri wa mtoni kupitia boti zenye injini moja.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *