Katibu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Vincent Mpwaji amewahimiza wanajamii kutowaficha watoto wenye ulemavu wa akili na badala yake wawasaidie kuwaunganisha na taasisi zinazowahudumia ili nao wafurahie haki yao ya kuishi na kufurahia maisha.
Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Kuwasaidia Watu Wenye Ulemavu ikiwemo wa Saikolojia cha Antonia Maria Verna, Kawe, Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, Balozi wa Italia nchini, Giuseppe Sean Coppola na Mkurugenzi wa taasisi ya COMSOL nchini Tanzania, Valentina Decao wamesema wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu waliopo katika jamii.
(Feed generated with FetchRSS)