#HABARI: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, ameanza ziara ya siku tisa katika mikoa ya Tabora na Kigoma, ambapo amepokelewa katika wilaya ya Igunga.
Katika mapokezi hayo Kihongosi ametawazwa kuwa chifu wa kabila la Wanyamwezi na kupewa jina la heshima la “Chifu Sali,” ishara inayozingatia imani na utamaduni wa wakazi wa eneo hilo katika kuimarisha mahusiano na viongozi.
Baada ya kutawazwa, viongozi hao wamezungumza na wakazi wa Igunga wakisisitiza umuhimu wa mshikamano na amani katika kuelekea harakati mbalimbali za maendeleo ya chama na serikali.
Ziara hiyo inalenga kukagua uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi, na kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mikoa hiyo ya Kanda ya Magharibi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.