Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema kuwa, uchokozi wowote mpya dhidi ya Iran utapelekea kuwaka moto katika eneo lote la Asia Magharibi.

Sheikh Maher Hamoud amesema hayo katika mahojiano na Mtandao wa Al-Nujaba na kubainisha kwamba, “Tathmini na mtazamo jumla na uliopo ni kwamba Marekani haitafanya upumbavu wa kushambulia Iran kwa sababu utawala wa Israel hauwezi kuvumilia kukabiliana na makombora kutoka Iran, Yemen, Iraq, na Lebanon. Iran ina uzoefu mkubwa na mpana katika nyanja za usalama na kijeshi ambao unazidi uzoefu wa nchi zingine. Vikosi vya kijeshi vya Iran viliweza kuangusha ndege isiyo na rubani ya kisasa zaidi ya Marekani awali, huku Wamarekani hawakuwa wakifikiria kitu kama hicho na uwezo kama huo kutoka kwa Iran.”

Sambamba na kubainisha kwamba Iran imepiga hatua nzuri katika uwanja wa teknolojia, aliongeza: “Katika Vita vya Siku 12, Wairani wote waliungana, na mshikamano huu ukawa moja ya sababu za ushindi.

Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema kuwa, kipengele muhimu zaidi cha nguvu ya Iran ni kuwepo kwa kiongozi wa kipekee, wa dhati, mwaminifu, mwenye nguvu, na mnyenyekevu, na adui anajua kwamba kiongozi huyu ndiye chanzo cha nguvu ya Iran.

Aidha Sheikh Maher ameeleza kuwa, moja ya nguzo zingine za nguvu ya Iran ni umoja wa kitaifa na mshikamano.

Pia alisema kuhusu uungaji mkono wa Iran kwa watu wa Palestina: “Tangu mwaka 1342 Hijria Shamsia, wakati Imam Khomeini (RA) alipoanza mapambano yake ya kupinga Uzayuni na kukabiliana na ubeberu, Iran haijaacha kuunga mkono na kuisaidia Palestina, na tunaamini uungaji mkono huu utaendelea hadi utawala dhalimu wa Israel utakapoangamizwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *