#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, imemhukumu Evarist Justin Chamtepa (44) kifungo cha miaka 30 jela, na kulipa fidia ya Shilingi Milioni 5 baada ya kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 14.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Denis Luwungo, alisema mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo na kwamba hukumu hiyo imetolewa baada ya kuzingatia ushahidi uliotolewa Mahakamani.
Shitaka la kesi namba 1615 linasema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya mzozo wa kifamilia, ambapo mkewe wa mtuhumiwa alikimbilia kwa wifi yake na kulala hapo usiku, na mtuhumiwa kutumia nafasi hiyo kutenda kitendo hicho.
Kesi ilihusisha makosa chini ya kifungu cha 130 (1) na kifungu cha 2(e) pamoja na kifungu cha 131(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) sura ya 16, marejeo ya mwaka 2023.
Baada ya Mahakama kujiridhisha na ushahidi na kuzingatia ombi la mtuhumiwa la kupunguzwa adhabu kwa sababu alikuwa amelewa wakati wa tukio, Hakimu Luwungo alimuhukumu kifungo cha miaka 30 jela na amemlazimisha kulipa fidia ya Shilingi Milioni 5 atakapomaliza kifungo chake.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.