Vyanzo vya usalama vimesema kwamba mashambulizi ya waasi wenye silaha yamewaua watu wasiopungua 10 kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso.

Burkina Faso, ambayo tangu Septemba 2022 inatawaliwa na baraza la kijeshi linaloongozwa na Kapteni Ibrahim Traore, imekuwa ikishuuhuudiwa ghasia zinazofanywa na makundi yenye uhusiano na al-Qaeda na Daesh kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Mashambulizi ya karibuni zaidi yalitokea Jumapili, wakati kikosi cha zimamoto kiliposhambuliwa kaskazini mwa nchi hiyo. Vyanzo havikutoa takwimu zozote za waathiriwa, lakini vimesisitiza kuwa lilikuwa shambulio “kubwa”.

Jumamosi iliyopita pia, kambi ya kijeshi ya Titao, mji mkuu wa jimbo la Loroum, kaskazini mwa Burkina Faso, ilishambuliwa na kundi la mamia ya wanaume waliokuwa na silaha.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa “taasisi za kiufundi” za kambi hiyo zimeharibiwa, bila kutaja idadi ya vifo au majeruhi.

Baraza la kijeshi mjini Ouagadougou halijatoa tamko lolote kuhusu mashambulizi hayo yanayyotokea mara kwa mara katika maeneo tofauti ya Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *