Barcelona, Hispania. Jina la mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane limeibuka katika kampeni ya kuwania Urais wa Barcelona kuelekea uchaguzi wa klabu hiyo utakaofanyika Machi 15, mwaka huu.

Xavier Vilajoana ameahidi kwamba iwapo atafanikiwa kuibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Klabu hiyo, atahakikisha Harry Kane mwenye umri wa miaka 32 anatua katika kikosi chao.

Inatajwa kuwa katika mkataba wa Harry Kane na Barcelona kuna kipengele kinachomruhusu mshambuliaji huyo kuuzwa kwa kiasi cha Pauni 52 milioni (Sh181 bilioni) na Vilajoana anaamini kuwa uongozi wake utaweza kukifikia na kumnasa nyota huyo ili awe mrithi wa Robert Lewandowski.

Vilajoana amesema kuwa tayari ameshawasiliana na upande wa Harry Kane na iwapo akichaguliwa tu kuwa Rais, mchezaji huyo atavaa jezi ya Barcelona.

“Tumeshafanya mawasiliano mara kadhaa na nadhani ni ambaye atakuwa fiti sana kutegemea hali ya mkataba wake.

“Kane ni mshambuliaji ambaye atamudu vilivyo aina yetu ya kiuchezaji. Ni mshambuliaji mwenye uwezo wa kushuka chini na kushiriki mchezo na wachezaji wenzake katika timu. Anaweza kucheza pia kama namba tisa, muuaji na mmaliziaji.

“Ni mchezaji anayeleta uhai uwanjani. Anaweza kucheza vyema pindi timu inapokaa nyuma. Anaweza kuongeza vingi katika uchezaji wa Barcelona,” alisema Vilajoana.

Vilajoana ametamba kuwa Kane ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitamani kuitumikia Barcelona hivyo kupatikana kwake kutakuwa ni jambo rahisi.

“Ninajua pia kuwa anaipanda Barcekina. Wapo wachezaji wachache ambao hawaipendi Barcelona. Kwa hiyo ni suala la kulizungumzia tu, bila shaka,” alisema mgombea huyo.

Uhamisho wa Harry Kane kutoka Tottenham Hotspur F.C. kwenda FC Bayern Munich umekuwa na mafanikio makubwa, na mkataba wake wa sasa na mabingwa hao wa Ujerumani unaendelea hadi mwaka 2027.

Rekodi yake ya kufunga mabao 109 katika mechi 126 ni ya kushangaza sana, lakini bado haijulikani kama atavutiwa na changamoto mpya katika Ligi Kuu Hispania au kurejea Ligi Kuu England.

Víctor Font Vilajoana ana uzoefu mkubwa sana na ana nafasi ndogo ya kushinda uchaguzi, ingawa Joan Laporta bado anaongoza kama mgombea mwenye nafasi kubwa zaidi.

Alikuwa sehemu ya kikosi kama mchezaji kabla ya kuingia katika uongozi wa klabu, ambako alihudumu chini ya Joan Laporta, Sandro Rosell, na Josep Maria Bartomeu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *