Jeshi la Mexico, hapo jana jioni lilitangaza kufanikiwa kumuua moja ya viongozi wa juu wa makundi ya dawa za kulevya nchini humo Nemesio “El Mencho” Oseguera, katika operesheni ambayo ilisababisha vurugu katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Oseguera aliyefahamika sana kwa jina la “El Mencho”, alikuwa kiongozi wa kundi la Jalisco New Generation na alijeruhiwa katika makabiliano na wanajeshi kwenye mji wa Tapalpa na alifariki akipelekwa hospitali, taarifa ya jeshi imesema.

Kiongozi huyo ambaye zamani aliwahi kuwa afisa wa juu kwenye jeshi la polisi, kwa muda mrefu alikuwa akisakwa na mamlaka za nchi hiyo pamoja na Serikali ya Marekani iliyokuwa imetangaza dau la dola milioni 15 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake.

Kufuatia tangazo la kifo chake, watu waliokuwa na silaha walifunga baadhi ya barabara kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwemo Jalisco na Tapalpa, wakichoma moto magari na malori ya mizigo.

Oseguera anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu zaidi wa makundi ya dawa za kulevya kuuawa nchini humo tangu kukamatwa kwa aliyekuwa muasisi wa kundi jingine linalofahamika kama Sinaola, Joaquin Guzman maarufu kama El Chapo na Ismael Zambada, ambao kwa sasa wao wanatumlikia kifungo katika jela za Marekani.

Nchi kadhaa ikiwemo Marekani na Uingereza, zimewataka raia wake kutotembea kwenye miji yenye vurugu, wakati huu safari kadhaa za ndege zikiwa zimesitishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *