Chad imetangaza kuwa, ili kuzuia kuenea mapigano kwenye maeneo ya mpakani, inaufunga mpaka wake wa pamoja na Sudan hadi itakapotolewa taarifa nyingine.

Serikali ya N’Djamena imeeleza katika taarifa kwamba uamuzi wa kufunga mpaka baina yake na Sudan umechukuliwa ili kuzuia mgogoro wa nchi hiyo ndani ya ardhi ya Chad, na kwamba nchi hiyo ina haki ya kujibu uchokozi wowote au ukiukaji wa mipaka na ardhi ya nchi hiyo.

Chaneli ya habari ya Cairo nayo pia imeripoti kadhia hiyo na kutangaza kwamba, bila kutoa taarifa kabla, Chad imefunga vivuko vya Al-Tina, Adri, Fourbaranga na Umm Dekhn kama hatua ya tahadhari ya kuzuia kushamiri mapigano ya silaha na kuenea hadi ndani ya ardhi ya Chad.

Chaneli ya Cairo imeongeza kuwa: siku ya Jumamosi, wanamgambo wa Sudan wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka waliwashambulia wanajeshi kadhaa wa Chad ndani ya ardhi ya nchi hiyo na kusababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi tisa, na kwamba ni baada ya hapo ndipo serikali ya Chad ikaamua kufunga mpaka.

Mapigano kati ya Jeshi la Sudan SAF na RSF yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 2023, chanzo kikiwa ni mzozo juu ya kuunganishwa wanamgambo wa RSF katika vikosi vya kawaida vya jeshi. Mgogoro huo umesababisha baa la njaa katika sehemu kadhaa za Sudan, kuzusha moja ya hali mbaya zaidi ya kibinadamu duniani, kupelekea kuuawa makumi ya maelfu ya watu na kuwalazimisha karibu watu milioni 13 kuyahama makazi yao …/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *