Willy Ngoma, ameuawa mapema leo Jumanne Februari 24 katika Mji wa Rubaya eneo la Masisi Kivu Kaskazini, afisa kutoka kwenye kundi la waasi wa M23 ameithibitishia RFI.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ngoma na wanachama wengine kutoka kwenye kundi hilo waliuawa katika hali ambayo hadi tukichapisha taarifa hii haikuwa imeeleweka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, msafara wa ngoma ulishambuliwa na ndege zisizo na rubani.

Mashambulio ya ndege zisizo na rubani yamekuwa yakiripotiwa katika Mji wa Rubaya tangu Jumatatu ya wiki hii, Februari 23.

Idadi ya watu wote waliouawa kwenye shambulio hilo hadi tukichapisha taarifa hii haikuwa imewekwa wazi.

M23 inaituhumu jeshi la DRC (FARDC) kwa kuimarisha mashambulio katika majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini katika kipindi cha siku 10 zilizopita.

Kulingana na M23, FARDC imekuwa ikitekeleza mashambulio mazito katika Mji wa Rubaya huko Masisi, eneo lenye utajiri wa madini muhimu ya coltan .

Willy Ngoma ambaye amekuwa nguzo muhimu kwa waasi wa M23 alitangaziwa vikwazo na Marekani mwezi Disemba mwaka wa 2023.

Kulinagana na Washington, alitangaziwa vikwazo kutokana na mchango wake kwa kundi la AFC-M23 ambalo limetekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji ya watu pamoja na ubakaji wa wanawake.

Marekani ilirejelea haswa ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa mwezi Novemba mwaka wa 2022 katika eneo la Kishishe, Kivu Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *