• Wanawake watatu wazee walinaswa na kamera za ulinzi wakiiba mafuta ya kupikia kutoka Optidrops Supermarket mjini Ngong mnamo Februari 19
  • Watatu hao walionekana kuratibu mienendo yao, wakiingia mmoja baada ya mwingine na kwa ustadi kuweka makontena kwenye mikoba yao bila kuonekana
  • Kwa kukosekana kwa wahudumu au wateja katika njia hiyo ya bidhaa, wanawake hao walitekeleza wizi huo wa kimya kimya bila kugunduliwa papo hapo

Wanawake watatu wazee waachunguzwa na duka moja mjini Ngong baada ya kamera za ulinzi kuwanasa wakiiba Alhamisi, Februari 19.

Wanawake hao waliingia Optidrops Supermarket jioni, wakitumia mwanya wa kutokuwepo kwa wahudumu katika njia ya bidhaa kuiba mafuta ya kupikia.

Waliingia mmoja baada ya mwingine kuchukua walicholenga kuiba, bila mtu yeyote kugundua kwa wakati huo.

Kwa kuzingatia namna walivyotekeleza operesheni yao, wanawake hao walionekana kuwa walipanga wizi huo wa kimya kimya na kuratibu mienendo yao ili kuepuka kugunduliwa.

Wa kwanza, aliyekuwa amevaa gauni la maua la rangi ya maruni, blaza jeupe na skafu nyekundu, alielekea mwisho wa njia iliyokuwa imejaa bidhaa za vyakula.

Pia soma

Willy Paul Anashiriki Ujumbe Mgumu, Vidokezo vya Kurudi kwenye Tasnia ya Injili

Alijifanya kutafuta bidhaa fulani, kisha akaangalia eneo lote kuhakikisha hakuna anayemtazama.

Alipiga magoti kidogo kuchukua kontena la mafuta ya kupikia, akaliweka kwenye mkoba wake na kuondoka haraka.

Kisha akafuata mwanamke wa pili, aliyeonekana kuwa mdogo kidogo kuliko wa kwanza.

Hakupoteza muda; aliangalia kama kuna kamera za ulinzi, na baada ya kujiridhisha kuwa hakuna iliyokuwa ikimwangalia, alichukua makontena mawili na kuyaweka kwenye mkoba wake kabla ya kuondoka muda mfupi baadaye.

Msururu wa wizi ulimalizika na mwanamke wa tatu, aliyekuwa amevaa gauni jeupe la maua na bleza ya njano.

Alielekea eneo hilo huku akijifanya kununua, akiangalia pande zote kuhakikisha hakuna anayewaangalia.

Aliona makontena mawili, akainama kuyachukua na kuyaweka kwenye mkoba wake kabla ya kuondoka katika njia hiyo.

Wakati wote huo, hakukuwa na mfanyakazi yeyote aliyekuwa akisimamia eneo hilo, wala hakukuwa na mteja mwingine aliyekuwa akinunua karibu.

Kulingana na mmiliki wa duka hilo, watatu hao hawakuiba tu mafuta ya kupikia bali pia bidhaa nyingine za vyakula na zisizo za chakula, zikiwemo taulo za kike.

Pia soma

Mkasa wa Ziwa Naivasha: Mama Mwenye Uchungu Ampoteza Mwanawe Aliyezama Akivua Samaki

Inaripotiwa kuwa walitoroka na bidhaa zenye thamani inayozidi Shilingi za Kenya 5,000.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *