Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa
Marekani Donald Trump ameonya nchi dhidi ya kujiondoa katika mikataba ya
kibiashara iliyojadiliwa hivi karibuni na Marekani baada ya Mahakama ya Juu
Zaidi nchini humo kutoa uamuzi kuwa ushuru wake wa dharura siyo halali,
akisema kwamba ikiwa watafanya hivyo, atawatoza ushuru mkubwa zaidi chini ya
sheria tofauti za kibiashara.
Trump,
katika mfululizo wa machapisho ya mitandao ya kijamii, alisema pia anaweza
kutoza ada za leseni kwa washirika wa kibiashara huku kutokuwa na uhakika
kuhusu hatua zake zijazo za ushuru kukiathiri uchumi wa dunia.
“Nchi
yoyote inayotaka ‘kucheza mchezo wa paka na panya’ na uamuzi wa kipuuzi wa
mahakama ya juu zaidi, hasa zile ambazo ‘zimeiibia’ Marekani kwa miaka mingi,
na hata miongo kadhaa, zitakabiliwa na ushuru wa juu na mbaya zaidi, kuliko ule
ambao wameukubali hivi karibuni. MNUNUZI TAHADHARI!!!” Trump aliandika
kwenye mtandao wa Truth Social.
Trump
alisema kwamba licha ya uamuzi wa mahakama wa kubatilisha ushuru wake chini ya
Sheria ya Dharura ya Kiuchumi Kimataifa, uamuzi wake umethibitisha uwezo wake
wa kutumia ushuru chini ya mamlaka zingine za kisheria “kwa njia yenye
nguvu zaidi na ya kuchukiza, kwa uhakika wa kisheria, kuliko ushuru kama
ulivyotumika awali.”
Alipendekeza
kwamba Marekani inaweza kutoza ada mpya za leseni kwa washirika wa kibiashara,
lakini hakutoa maelezo yoyote.
Msemaji wa
ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani hakujibu mara moja ombi la kutoa
maoni zaidi kuhusu mipango ya Trump.
Pia unaweza kusoma: