Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la AFP, umebaini kuwa serikali ya Nigeria iliwalipa mamilioni ya dola za Marekani wanajihadi wa kiislamu wa kundi la Boko Haram ili kuwaachia watoto 230 pamoja na wafanyakazi wao waliotekwa kwenye shule moja ya kanisa katoliki mwezi Novemba mwaka jana.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za Kiintelijensia, zimebaini kuwa serikali ya Nigeria ilitoa mamilioni ya Dola kama kikombozi ili wanafunzi hao kuwa huru, na kwamba Mbali na pesa hizo, serikali pia iliwaachia huru makamanda wawili wa Boko Haram, kitendo ambacho anaharakati wanasema ni kinyume cha sheria ya nchi hiyo.

Taarifa zinasema,  fedha hizo zilisafirisha kwa Helikopta hadi katika ngome ya Boko Haram ya Gwoza, kwenye jimbo la Borno karibu na nchi jirani ya Cameroon, na kwamba  zilikabidhiwa kwa Ali Ngulde, Kamanda wa Boko Haram, kwa mujibu wa watu watatu waliozungumza na AFP, ambapo baada ya kupokea fedha hizo, alivuka nchini Cameroon, kabla ya wanafunzi hao kuachiwa huru.

Hata hivyo serikali ya Nigeria, imeendelea kusisitiza kuwa haijawahi na huwa haiwalipi magaidi na wanajihadi ili wawaachilie mateka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *