
Nchini Senegal, Waziri Mkuu Ousmane Sonko amewasilisha bungeni sheria mpya, inayotoa adhabu kali kwa watu wanaojihusisha na vitendo na mapenzi ya jinsia moja katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya, yeyote atakayepatikana na hatia hiyo, atafungwa jela miaka 10.
Haya ni marekebisho kwenye sheria inayotumika kwa sasa ambayo inatoa adhabu ya miaka mitano, ambayo imekuwa ikishtumiwa na watetezi wa haki za binadamu.
Aidha, serikali inataka pia hatua kali kuchukuliwa kwa wale watakaojihusisha na vitendo hivyo dhidi ya watoto.
Wale wanaohamasisha vitendo hivyo, watahukumiwa jela kati ya miaka mitatu hadi miaka saba.
Mswada huo wa sheria umepelekwa bungeni baada ya kupitishwa na Baraza la Mawaziri wiki iliyopita, na inakuja pia baada ya mwezi huu, polisi kuwakamata wanaume saba, akiwemo mwanahabari maarufu kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Tarehe ya wabunge kupigia kura mswada huo wa sheria, bado haijatangazwa.