Tume ya Ushindani (FCC), imeingia rasmi katika matumizi ya Mfumo wa Serikali wa Ukaguzi wa Bidhaa kwa Pamoja (TANOGA) ili kupambana na uingizwaji wa bidhaa bandia.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na Tume hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa FCC, Salvor Chuwa amesema lengo la kuingia Katika mfumo huo ni kuhakikisha nchi inakuwa na mazingira salama na rafiki kibiashata.

Amesama mfumo huo wa kidigitali utawawezesha wamiliki wa nembo za bidhaa kupata thamani halisi ya uwekezaji wao.

“Mfumo huu pia utahakikisha walaji wanalindwa ili wapate thamani halisi ya bidhaa wanazotumia yenye kukidhi marajio yao.,”

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa amesema kuwa Tume hiyo imefanya marekebisho ya Sheria ili kufikia malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua milango kwa wawekezaji na kukuza biashara.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Khadija, mpango huu unafaida kubwa kwa Taifa. Unalinda usalama wa watumiaji, unaimarisha ushindani wa haki kwa biashara halali, unaongeza mapato ya Serikali kwa kupunguza ukwepaji wa kodi na kuongeza imani kwa wawekezaji .

Chuwa ameongeza kuwa kwa sasa Tume ya FCC inaendelea na utekelezaji wa miradi miwili ya kidigitali ambayo ni Daftari la Kieletroniki la Alama za Biashara na Tovuti ya Maombi ya Alama za Biashara inayorahisisha uwasilishaji, mapitio uhuishaji wa maombi kwa njia ya mtandao.

Akifungua mkutano huo , Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesisitiza Tume ya Ushindani (FCC), Kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo waandishi wa habari ili kudhibiti bidhaa bandia nchini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *