Waangalizi kutoka kwenye Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wamewasili mjini Uvira, tayari kuanza kazi ya kuthathmini  utekelezwaji wa usitishwaji wa vita kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23/AFC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya pande zote kukubaliana kuwa, waangalizi kutoka MONUSCO, kwenda mjini Uvira ili kuangalia namna pande zote zinavyotekeleza makubaliano ya kuacha vita katika mji huo uliopo, jimboni Kivu Kusini.

Aidha, hii inakuja baada ya waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda, kuuvamia mji huo mwezi Desemba mwaka uliopita, lakini wakaondoka mwezi Januari baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani.

Mbali na waangalizi kutoka MONUSCO, kuna waangalizi wengine kutoka jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu, ambao watakuwepo kwenye mji huo hadi siku ya Ijumaa.

Waangalizi hao watakuwa na kazi ya kuthathmini hali ya usalama mjini Uvira, hali ya watu kuingia na kutoka kwenye mji huo hatua ambayo inalenga kuwa na waangalizi wa muda mrefu watakaokuwa na kazi ya kusimamia usitishwahji wa vita Mashariki mwa DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *