Wananchi wa kijiji cha Fela wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaoishi kwenye maeneo yanayopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha tano, Mwanza–Isaka, wameiomba serikali kuzingatia ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kilimo na ufugaji bila vikwazo.
Ombi hilo wamelitoa mbele ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo uliofikia asilimia 68.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)