Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Armenia kuhusu azma ya Iran ya kustawisha na kuimarisha uhusiano wa pande mbilii na majirani zake hasa Armenia.
Katika mazungumzo hayo na Suren Papikyan Waziri wa Ulinzi wa Armenia na ujumbe aliofuatana nao ziarani hapa Tehran; Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuhusu mtazamo mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na matukio ya kikanda na kueleza kuwa: Sera madhubuti ya Iran ni kuunga mkono amani, utulivu na usalama endelevu katika eneo hili, na hatuna lengo la kuibua machafuko kwa hali yoyote ile kwa sababu ukosefu wowote wa amani utaziathiri nchi zote za kanda hii.
Rais wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kukamilisha “Hati Kamili ya Ushirikiano wa Kistratejia” kati ya Tehran na Yerevan na kubainisha kuwa: Maslahi ya nchi mbili yatadhaminiwa pakubwa kadiri pande mbili zitakavyoweza kuboresha kiwango cha uhusiano kati yao katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, usafirishaji, nishati na miundombinu.
Meja Jenerali Abdulrahim Mousavi Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran pia amesisitiza katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Armenia kwamba Iran iko tayari kustawisha ushirikiano wa kijeshi na vikosi vya ulinzi vya Armenia. Brigedia Jenerali Rubani Aziz Nasirzadeh Waziri wa Ulinzi wa Iran pia amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Armenia na kuashiria uhusiano mkubwa wa kihistoria na kimkakati kati ya nchi mbili na kusisitiza kuwa Tehran inapinga mabadiliko yoyote ya kijiopolitiki katika eneo la Magharibi mwa Asia na uingiliaji wa nchi ajinabi.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka ya karibuni imeelekeza ushirikiano wake katika sera ya utangamano wa kikanda. Mazungumzo ya karibuni katii ya Rais wa Iran na Waziri wa Ulinzi wa Armenia pia yanaweza kuchambuliwa katika fremu hiyo. Iran nchi iliyo na nafasi muhimu ya kijiopolitiki katika eneo la Magharibi mwa Aasia na mpaka kati ya Kafkaz, Ghuba ya Uajemi na Asia ya Kati inatambua kuwa usalama wa kanda h ii ni muhimu kwa usalama wake wa taifa. Kwa msingi huo sisitizo la Pezeshkian la kuimarisha uhusiano na nchi jirani khususan Armenia ni katika sera ambazoo lengo lake ni kuleta uwiano, kuzuia migogoro na kudumisha amani endelevu ya kikanda.
Ushirikiano wa kiulinzi na kiusalama; kudhamini amani na ustawi, na ushirikiano wa kiulinzi kati ya Iran na Armenia katika miaka ya hivi karibuni pia unaashiria uelewa wa pamoja wa nchi hizi mbili kuhusu vitisho vya kieneo na umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiusalama kati yazo.
Aidha mazingira ya kujipenyeza na kuwepo madola ajinabi yatapungua kwa kuimarishwa ushirikiano wa ndani kati ya nchi za kanda hii. Wakat huo huo uratibu wa kilulinzi kati ya Iran na nchi majirani zake pia unaweza kuwa na nafasi athirifu mkabala wa harakati haribifu. Aidha, kuwepo usalama wa kutosha ni sharti kuu la kuimarika na kustawi kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kuimarisha sekta ya uchumi katika eneo.
Kwa kuwa na nafasi nzuri ya kijiografia; Iran inataka kuimarisha nafasi yake ya kiuchumi na usafirishaji kupitia korido za kimataifa za usafirishaji, kama vile njia ya Kaskazini-Kusini, na Mashariki-Magharibi. Ushirikiano wa karibu kati ya Iran na Armenia unaweza nakuwa na nafasi kuu katika uwanja huu.
Njia ya Iran- Armenia inaweza kutumika kama daraja la mawasiliano ya kuaminika kati ya masoko ya Russia, Asia ya Kati na Ghuba ya Uajemi. Mfungamano kama huu utaanda uwanja wa kupatikana amani ya kudumu kati ya nchi mbalimbali kwa sababu maslahi ya pamoja ya kiuchumi yanazuia kuibuka mizozo na yanastawisha ushirikiano wa pande kadhaa. Wakati huo huo kuendelezwa korido huru za kikanda kutoa msukumo kwa nchi za eneo hili kufuata sera zao za kiuchumi na kimkakati kwa uhuru zaidi.
Mazungumzo na mashauriano ya karibuni kati ya viongozi wa Iran na wenzao wa Armenia yanapasa kuzingatiwa kuwa ishara ya mabadiliko katika sera za kikanda za Tehran; tukio ambalo linadhihirisha stratejia ya pande kadhaa na ya busara katika ngazi ya kisiasa, kusalama na kiuchumi.
Stratejia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itajikita katika kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kijeshi kwa lengo la kuzuia migogoro na kukabiliana na uingiliaji wa nchi ajinabi; kupanua uhusiano wa kiuchumi, nishati na usafiri ili kuwa na mahusiano athirifu; kuanzisha miundombinu ya mawasiliano na korido za kikanda kama nguzo za amani na ustawi endelevu; na kuimarisha nafasi ya Iran kama mhimili wa amani na utulivu katika kanda hii.