Polisi ya Benin imetenga kitita cha faranga za CFA Milioni 20 kwa atakaye saidia kukamatwa kwa wahusika wakuu wa mapinduzi yaliyoshindwa ya Desemba 7. Taarifa hii imegonga vichwa vya habari na kusambazwa kweye mitandao ya kijamii tangu siku ya Jumatatu, Machi 2.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan

Karibu miezi mitatu baada ya jaribio la mapinduzi ya Desemba 7, ambalo lililenga kumpindua Rais Patrice Talon, polisi wa Benin bado wanawatafuta wahusika.

Baada ya kutoa hati za kimataifa za kuwakamata, polisi wamekuwa wakisambaza notisi ya kuwasaka kwa siku kadhaa, wakitoa zawadi kubwa kwa yeyote anayetoa taarifa kubwa kupiti simu na inayoweza kuthibitishwa kwa simu ambayo itasaidia kukamatwa kwa watu wahusika wa jaribio la mapinduzi lililoshindwa ambao wanatafutwa kwa udi na uvumba. Polisi wanahakikisha atakayetoa taarifa hiyo hataweza kujulikana.

Tangu Jumatatu, Machi 2, haswa, taarifa hiyo imegonga vichwa vya habari nchini Benin na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Zawadi hiyo imewekwa kuwa faranga milioni 20 za CFA, sawa na zaidi ya euro 30,000.

Kanali Pascal Tigri anaonyeshwa akiwa amevaa nguo za kiraia na sare za kijeshi

Notisi hiyo ina picha za watu tisa wanaotafutwa wenye majina yao kamili. Anayetambulika zaidi ni Kanali Pascal Tigri. Akichukuliwa kuwa mhusika mkuu wa mapinduzi yaliyoshindwa, anaonyeshwa akiwa na sura mbili: kwanza akiwa amevaa nguo za kiraia, kisha akiwa amevaa sare za kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *