
Nchini Guinea, serikali imejaribu kuzima uvumi unaoebdelea nchini humo. Baada ya kuwa nje ya nchi kwa wiki mbili na nusu, “Rais Mamadi Doumbouya anaendelea vizuri,” Waziri Mkuu Amadou Oury Bah ameiambia RFI jioni ya Jumatatu, Machi 2. Mkuu wa nchi, akionekana amechoka kulingana na washauri wake, yuko nje ya nchi akipumzika na anapaswa kurudi Guinea ndani ya wiki moja, kulingana na ofisi ya Waziri Mkuu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mamadi Doumbouya ambaye aliondoka Februari 13 kushiriki katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, hajarudi Guinea tangu ziara hii rasmi. Kutokuwepo huku kwa muda mrefu kumefanya mamlaka kutoa tamko wakati serikali ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake imeundwa.
Waziri Mkuu Amadou Oury Bah amebaini kwamba Mkuu wa Nchi, ambaye aliwasiliana naye siku ya Jumatatu asubuhi, anaendelea vizuri: “Ninaweza kuthibitisha, na lazima niseme kwamba tulizungumza asubuhi ya leo [Jumatatu, Machi 2]. Yuko sawa. Hata kama yuko mbali ya nchi, anafuatilia habari za nchi kila wakati. Anajua mambo yote muhimu ya maisha ya nchi. Kama binadamu yeyote, kuna nyakati ambapo mtu anaweza kuhisi amechoka. Unajua, kipindi cha mpito cha miaka minne iliyopita, pamoja na mvutano uliokuwa ukiendelea pande mbalimbali, wakati mwingine unahitaji kupumzika ili kupumua, kujianda upya, na kurudi akiwa na nguvu zaidi. Hilo ndilo Rais Doumbouya anafanya kwa sasa.”
Ili kumruhusu Mkuu wa Nchi kupumzika kwa amani, mamlaka zinakataa kutaja nchi aliko. Waziri Mkuu Amadou Bah Oury amesema kwamba Mamadi Doumbouya atarudi Guinea “Mungu akipenda, ndani ya wiki moja.”