.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erling Halaand

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amekuwa kivutio kikuu kwa rais wa Barcelona Joan Laporta, ambaye ana uhakika mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 25, atajiunga na klabu hiyo ya La Liga siku zijazo. (El Nacional – In Spanish),

Manchester City wako tayari kushindana na Liverpool kwa ajili ya kumsajili bila malipo mlinzi wa England na Crystal Palace Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao, mkataba wake utakapokamilika. (Mirror)

Brentford wameonyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa pembeni wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 Almugera Kabar. (Bild – In Deutch, Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mark Guehi

Everton itakataa mbinu zozote za kumnunua beki wa kati wa England Jarrad Branthwaite 2026 huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akiwa sehemu ya mradi wa muda mrefu katika klabu hiyo. (Talksport)



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *