Dar es Salaam. Yanga, Azam na Singida Black Stars, bado zina nafasi ya kuitetea Tanzania kwenye michuano ya CAF katika kuwania nafasi ya kufuzu robo fainali, hiyo ni baada ya Simba hesabu kwenda vibaya.

Wikiendi hii, kazi inaendelea kwa wawakilishi wetu hao kujitupa uwanjani kusaka ushindi ambao utatoa picha halisi ya safari ya robo fainali. Unaweza kusema siku ya hukumu.

Ni mechi ambazo unaweza kusema ni fainali kwa sababu ya misimamo ya makundi yao ilivyo.

Pointi tatu za lazima

Siku ya leo itahitimishwa na mechi hii itakayoanza saa 4:00 usiku ambapo inazihusisha timu zilizolingana pointi katika kundi B la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kitendo cha Yanga kushinda 1-0 nyumbani dhidi ya AS FAR Rabat katika mechi ya kwanza, kimebeba matumaini makubwa ya kufanya vizuri mechi hii ambayo hata sare inawabeba.

Mabingwa wa Afrika, Al Ahly inaongoza ikiwa na pointi nane, inafuatia Yanga (5), kisha AS FAR Rabat (5), huku JS Kabylie ikiburuza mkia ikikusanya pointi mbili.

Katika kundi hili, timu zote

zina nafasi ya kufuzu robo fainali kulingana na pointi zilivyo, lakini JS Kabylie ina kazi kubwa ya kufa nya ili kutoboa kwani mechi mbili zilizobaki dhidi ya Al Ahly (nyum bani) na Yanga (ugenini) ishinde zote, kisha iombe Yanga na AS FAR Rabat zisipate pointi tatu.

Ushindi wa Yanga ni muhimu leo kwani ikifanya hivyo, itarudi nyumbanu kukamilisha ratiba tu huku ikiwa imeshafuzu robo fainali.

Matumaini ya Yanga yanakuja kutokana na kikosi hicho kuimarika siku hadi siku hasa baada ya maingizo mapya kipindi cha dirisha dogo la usajili akiwamo Laurindo Depu, Mohamed Damaro na Allan Okello, huku Buba Jameh akisubiriwa kuonyesha makali yake.

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema: “Tuna kazi ya kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mechi zetu mbili zijazo tukianza na FAR Rabat, tunatakiwa kwenda na akili ya ushindi.

 “Mechi hii dhidi ya Rabat ni sawa na kwamba tunakwenda kucheza fainali kuamua safari yetu ya kwenda hatua inay ofuata, tukijua kwamba tukishinda tutafuzu.”

Azam ndani ya mtihani mzito

Mechi hii itakayoanza saa 1:00 usiku imekaa kimtego, Dimba la New Amaan Complex lililopo Unguja, linaweza kuamua Azam ikaribie kufuzu robo fainali au safari iishie hapo.

Hiyo inatokana na kwamba, hivi sasa Azam inashika nafasi ya tatu kundi B la Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi sita, inazidiwa tatu na mpinzani wake AS Maniema yenye tisa ikikamata nafasi ya pili. Kinara ni Wydad yenye tisa pia, huku Nairobi United ikiburuza mkia, haina pointi.

Azam ili iweke hai matumaini ya kufuzu robo fainali, lazima iiachape AS Maniema na kufikisha pointi tisa, lakini ikitoa sare au kufungwa, mambo yatabadilika na safari yao itaishia hapo ikisubiri kukamilisha ratiba mechi ya mwisho.

Wakati Azam inacheza na Maniema, mapema saa 10:00 jioni, Wydad itaifuata Nairobi United, timu ambayo imepoteza mechi zote nne ilizocheza ikifungwa nyumbani na ugenini.

AS Maniema hata ikipoteza mechi ya leo, bado ina nafasi ya kujiuliza itakapoikaribisha Nairobi United katika mechi ya mwisho, baada ya ile kwanza ilipoifuata nchini Kenya kushinda 1-0.

Azam ina kazi ya ziada ya kufanya kwani mechi ya kwan za ilifungwa 2-0 ilipoifuata AS Maniema, hivyo kutokana na kanuni zilivyo, Azam ili ikae juu ya Wakongomani hao, inatakiwa kushinda kwa tofauti ya mabao 3-0.

Wydad imebakisha hatua chache za kufuzu robo fainali, ikishinda dhidi ya vibonde Nairobi United wanaoburuza mkia bila pointi, itakuwa imefuzu.

Ikitokea imezikosa pointi tatu za mechi hiyo, itahitaji moja pekee mbele ya Azam katika mechi ya mwisho itakayochezwa nchini Morocco ilifuzu, hivyo Waarabu hao suala la kufuzu hatua inayofuata, limekaa vizuri kulinganisha na washindani wake katika kundi B la Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa kutambua umuhimu wa mechi hii, Kocha wa Azam, Florent Ibenge amesema wamejipanga kwa mambo mawili, kulipa kisasi cha kufungwa ugenini, pili kutengeneza njia ya kufuzu robo fainali.

“Nimewaambia wachezaji wangu wanataki wa kucheza kama fainali mchezo huo ili washinde na waandike historia mpya na kwenda kutafuta pointi.

“Hii ni mechi ya kwenda kulipa kisasi kwani Maniema walitamba kwenye uwanja wa kwao na sasa ni zamu yetu, hivyo hakuna cha kutuzuia kushinda.

“Wapinzani wote waliosalia katika mechi zilizobaki walitufun ga katika michezo ya kwanza, ila huu ambao utakuwa wa mwisho kwenye uwanja wetu wa nyumbani ndio wa kufa au kupona ili kupata alama tatu muhimu.”

Kile kitendo Simba kupata sare ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Esperance wikiendi iliyopita, ndiyo imeondoa matumaini ya timu hiyo kufuzu robo fainali kwa mara ya nane katika michuano ya CAF ndani ya misimu tisa kuanzia 2017-2018.

Kucheza mechi nne na kukusanya pointi moja, ni matokeo mabaya kuwahi kuyapata Simba hatua ya makundi michuano ya CAF.

Inaposhuka dimbani leo saa 1:00 usiku dhidi ya Petro Atletico, timu iliyoshinda 1-0 ilipokuja kucheza na Simba, inaonesha ni kama itakuwa mechi ya upande mmoja.

Kund D la Ligi ya Mabingwa Afrika linaloongozwa na Stade Malien yenye pointi 8, huku Esperance ikifuatia na sita, kisha Petro Atlet ico (5), Simba ina moja ikiwa mkiani.

Kwa mujibu wa benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na Kocha Mkuu, Steve Barker, hivi sasa wanazitumia mechi hizo za CAF kuendelea kuimarisha kikosi kwani kuna mashindano mengine yanawakabili yakiwamo Ligi Kuu Bara na Kombe la FA ambayo wanahitaji kuyabeba baada ya kuyakosa kwa takribani misimu minne, Yanga ikitawala kwa kubeba mara zote hizo.

Petro Atletico ipo nyumbani leo kucheza na Simba, ushindi kwao ni wa muhimu zaidi kuliko wapinzani wao kwani utaifikisha hadi pointi nane ilizonazo Stade Malien hivi sasa inayoikaribisha Esperance.

Simba hesabu zao za kufuzu robo faibali zilifia Dar es Salaam ilipotoka 2-2 na Esperance, hii inatokana na idadi ya mechi zilizobaki na pointi ilizokusanya kwani hata ikishinda mbili zilizobaki itaishia pointi saba ambazo Esperance na Petro Atletico inaweza kuzifikia au kuzipita kabisa kutokana na ratiba ilivyo. Mechi ya mwisho Esperance dhidi ya Petro Atletico kitendo cha ikiisha kwa matokeo yoyote Simba haitakuwa na nafasi, ndio imezima kabisa ndoto za Wanamsimbazi.

“Ni kweli tumepoteza nafasi ya kufuzu lakini Simba ni klabu kubwa, tunapaswa kucheza kwa ajili ya heshima ya nembo, klabu na mashabiki wetu,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema kuwa mechi ya Petro Atletico ni muhimu kwa kikosi chake kwa sababu inatoa fursa ya wachezaji kuonesha tabia ya ushindani, nidhamu na kujituma, mambo ambayo ni msingi wa klabu kubwa kama Simba.

“Tuliumia sana hasa katika mechi iliyopita tulitegemea pengine tungebadili kitu. Ilikuwa mechi muhimu kwetu na tulitarajia matokeo mazuri lakini soka lina changamoto zake,” alisema kocha huyo.

Kwa mujibu wa Barker, matokeo hayo yameathiri kisaikolojia kikosi chake, lakini alisema bado anaona dalili za kupambana kwa wachezaji wake, jambo linalompa matumaini kuelekea michezo iliyobaki.

“Hata kama matokeo hayakuwa mazuri, nimeona wachezaji wakipambana. Hilo ndilo jambo muhimu kwangu kama kocha,” alisema.

Hata hivyo, Barker alisema mechi zilizobaki hazipaswi kuonekana kama za kukamilisha ratiba, bali kama fursa ya kujenga heshima na kujiandaa kwa misimu ijayo ya mashindano ya kimataifa.

Kocha huyo pia aliwataka wachezaji wake wakongwe kama Shomary Kapombe kuchukua jukumu la kuwaongoza vijana, akisema uzoefu wao unahitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho timu inahitaji mshikamano na nidhamu.

Barker alisema matokeo mazuri dhidi ya Petro Atletico yatakuwa na maana kubwa kwa Simba, kwani yatarejesha imani ya mashabiki na kuipa timu morali katika michezo ijayo ya mashindano, ikiwemo Ligi Kuu.

Mtihani kwa Singida

Kesho Jumapili ni mechi moja pekee ya mwakilishi wetu itachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan complex, Unguja ambapo Singida Black Stars yenye pointi nne itaikaribisha CR Belouizdad.

Licha ya Singida Black Stars kuburuza mkia, lakini kama ikichanga vizuri karata zake inatoboa, inachotakiwa ni kushinda mechi hii ya nyumbani dhidi ya vinara wa kundi C la Kombe la Shirikisho Afrika, CR Belouizdad iliyokusanya pointi tisa.

Mechi nyingine itazikutanisha AS Otoho yenye pointi sita ikishika nafasi ya pili itaka pokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Stellen bosch iliyokusanya pointi nne ikikamata nafasi ya tatu.

Singida Black Stars ina kazi ya kufanya kwani mechi ya kwanza ilipok wenda Algeria, ilifungwa 2-0.

Singida Black Stars ikiuvuka mtihani huu, inapaswa pia kuichapa Stellenbosch mechi ya mwisho ili imalize kundi na pointi kumi zina zoweza kuivusha endapo AS Otoho na Stellen bosch zikipoteza angalau mechi moja tu kati ya mbili zilizobaki.

Uimara wa Singida Black Stars uwanja wa nyumbani ikiwa haijapoteza kufuatia kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Stellenbosch na kuichapa AS Otoho 1-0, kinaleta matumaini ya kuikanda pia CR Belouizdad, hivyo inapokwenda Afrika Kusini mechi ya mwisho kucheza na Stellebosch, ni fainali yao.

Kund D la Ligi ya Mabingwa Afrika linaloongozwa na Stade Malien yenye pointi 8, huku Esperance ikifuatia na sita, kisha Petro Atlet ico (5), Simba ina moja ikiwa mkiani.

Kwa mujibu wa benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na Kocha Mkuu, Steve Barker, hivi sasa wanazitumia mechi hizo za CAF kuendelea kuimarisha kikosi kwani kuna mashindano mengine yanawakabili yakiwamo Ligi Kuu Bara na Kombe la FA ambayo wanahitaji kuyabeba baada ya kuyakosa kwa takribani misimu minne, Yanga ikitawala kwa kubeba mara zote hizo.

Petro Atletico ipo nyumbani leo kucheza na Simba, ushindi kwao ni wa muhimu zaidi kuliko wapinzani wao kwani utaifikisha hadi pointi nane ilizonazo Stade Malien hivi sasa inayoikaribisha Esperance.

Simba hesabu zao za kufuzu robo faibali zilifia Dar es Salaam ilipotoka 2-2 na Esperance, hii inatokana na idadi ya mechi zilizobaki na pointi ilizokusanya kwani hata ikishinda mbili zilizobaki itaishia pointi saba ambazo Esperance na Petro Atletico inaweza kuzifikia au kuzipita kabisa kutokana na ratiba ilivyo. Mechi ya mwisho Esperance dhidi ya Petro Atletico kitendo cha ikiisha kwa matokeo yoyote Simba haitakuwa na nafasi, ndio imezima kabisa ndoto za Wanamsimbazi.

“Ni kweli tumepoteza nafasi ya kufuzu lakini Simba ni klabu kubwa, tunapaswa kucheza kwa ajili ya heshima ya nembo, klabu na mashabiki wetu,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema kuwa mechi ya Petro Atletico ni muhimu kwa kikosi chake kwa sababu inatoa fursa ya wachezaji kuonesha tabia ya ushindani, nidhamu na kujituma, mambo ambayo ni msingi wa klabu kubwa kama Simba.

“Tuliumia sana hasa katika mechi iliyopita tulitegemea pengine tungebadili kitu. Ilikuwa mechi muhimu kwetu na tulitarajia matokeo mazuri lakini soka lina changamoto zake,” alisema kocha huyo.

Kwa mujibu wa Barker, matokeo hayo yameathiri kisaikolojia kikosi chake, lakini alisema bado anaona dalili za kupambana kwa wachezaji wake, jambo linalompa matumaini kuelekea michezo iliyobaki.

“Hata kama matokeo hayakuwa mazuri, nimeona wachezaji wakipambana. Hilo ndilo jambo muhimu kwangu kama kocha,” alisema.

Hata hivyo, Barker alisema mechi zilizobaki hazipaswi kuonekana kama za kukamilisha ratiba, bali kama fursa ya kujenga heshima na kujiandaa kwa misimu ijayo ya mashindano ya kimataifa.

Mtihani kwa Singida

Kesho Jumapili ni mechi moja pekee ya mwakilishi wetu itachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan complex, Unguja ambapo Singida Black Stars yenye pointi nne itaikaribisha CR Belouizdad.

Licha ya Singida Black Stars kuburuza mkia, lakini kama ikichanga vizuri karata zake inatoboa, inachotakiwa ni kushinda mechi hii ya nyumbani dhidi ya vinara wa kundi C la Kombe la Shirikisho Afrika, CR Belouizdad iliyokusanya pointi tisa.

Mechi nyingine itazikutanisha AS Otoho yenye pointi sita ikishika nafasi ya pili itakapokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Stellen bosch iliyokusanya pointi nne ikikamata nafasi ya tatu.

Singida Black Stars ina kazi ya kufanya kwani mechi ya kwanza ilipokwenda Algeria, ilifungwa 2-0.

Singida Black Stars ikiuvuka mtihani huu, inapaswa pia kuichapa Stellenbosch mechi ya mwisho ili imalize kundi na pointi kumi zina zoweza kuivusha endapo AS Otoho na Stellen bosch zikipoteza angalau mechi moja tu kati ya mbili zilizobaki.

Uimara wa Singida Black Stars uwanja wa nyumbani ikiwa haijapoteza ndiyo nguzo yao leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *