Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi jana amezungumza kwa simu na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na pia na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya kujadili kadhia ya nyuklia na kuondoa vikwazo haramu na kusema: Wakati umefika sasa kwa nchi za Ulaya kudhihirisha nia ya dhati na ya kweli katika diplomasia.

Araqchi amemetllia mkazo kuhusu msimamo thabiti na mkuu wa Iran katika kudumisha mazungumzo na diplomasia kama nyenzo muhimu za kuzuia kushtadi mivutano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa vikali hatua ya karibuni ya nchi tatu za Ulaya (E3) ya  kurejesha vikwazo vilivyoondolewa hapo awali na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa chini ya utaratibu wa Snapback mechanism wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaja hatua hiyo ya nchi tatu za Ulaya kuwa isiyoweza kuhalalishwa kisheria wala kimantiki. 

Sayyid Abbas Araqchi amezitaka pande za Ulaya kustafidi na fursa iliyopo ili kudumisha mkondo wa kidiplomasia na kuepuka mgogoro unaoweza kuzuilika. “Ni wakati sasa kwa upande wa pili kudhihirisha nia ya dhati na ya kweli katika diplomasia.

Araqchi amesisitiza kuwa Iran iko tayari kufikia utatuzi wa haki na  wenye wa uadilifu kwa maslahi ya pande zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *