Wanaharakati wawili wa nchini Kenya, Bob Njagi na Nicholas Oyoo, wameripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda katika mazingira ya kutatanisha. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wawili hao  inasemekana walitekwa na watu wanne waliokuwa wamejihami kwa bunduki na walioaminika kuwa maofisa wa usalama, ambapo waliingizwa kwa nguvu kwenye gari na baadae simu zao kuzimwa.

Rafiki aliyenusurika, amesema tukio hilo linahusishwa na wawili hao kumuunga mkono Bobi Wine, ambapo wakati wakikamatwa walikuwa sehemu ya msafara wa kampeni wa mwanasiasa huyo.

Video zilizorekodiwa wakati wa kampeni ya  Bobi Wine katika wilaya ya Kamuli mashariki mwa Uganda, zinaonesha Bob Njagi ambaye ni kiongozi wa Free Kenya Movement akiwa jukwani na Bobi Wine.

Utekaji huo unajiri miezi minne kupita tangu mwanaharakati wa Kenya Bonface Mwangi na mwenzake wa Uganda  Agather Atuhaire watekwe nyara nchini Tanzania  na kisha kutupwa katika mipaka ya nchi zao ambapo baadae walidai kuteswa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo vile vya kingono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *