a

Chanzo cha picha, Bunge

    • Author, Na Yusuph Mazimu
    • Nafasi,

Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limehitimisha rasmi shughuli zake Juni 27, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye pia alilitunuku hotuba ya mwisho. Litavunjwa rasmi Agosti 03 litakapohitimisha ukomo wake kikatiba.

Moja ya mafanikio makubwa ya bunge hili ni kuulizwa kwa maswali zaidi ya 20,300, kupitishwa kwa miswada 58, maazimio 922 na mikataba 12 ya kimataifa, likiwemo azimio la pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wa mfano.

Bunge hili lilianza rasmi Novemba 1, 2020, likifunguliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Hivyo kuingia kwenye historia ya kuhutubiwa na marais wawili tofauti. Kuhitimishwa kwa bunge na kuvunjwa kwake kunafungua njia rasmi ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kama ilivyo kwa mabunge yaliyotangulia, Bunge la 12 pia limeacha historia yake ya kipekee, likiwa na matukio ya kisiasa, kisheria na kijamii ambayo yataendelea kukumbukwa kwa muda mrefu.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *