#HABARI: Zaidi ya wananchi 30 wa Mtaa wa Majengo, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, waliotoa maeneo yao ya mashamba kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Trena ya kisasa SGR, wamelalamikia kucheleweshwa kulipwa malipo yao toka waliposaini mikataba mwaka 2023 jambo ambalo wanadai limepelekea wao kuishi kwa shida .
Wakiongea huku wakionyesha mashamba na nyraka zao wamedai kuwa kutokana na mkataba walitakiwa kulipwa miezi sita baada ya kuingia mkataba, lakini tokea mwaka 2023 hadi sasa bado hawajalipwa na kulazimika baadhi yao kufikisha malalamiko yao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni .
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania