#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bw#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bw

#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bw. Raymond Mndolwa, amewataka watumishi wapya wa NIRC kutumia maarifa na ujuzi walionao ili kufanikisha malengo ya Tume na kuzingatia uadilifu katika utendaji. Amesema kila mtumishi ana nafasi ya kipekee katika utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo, hivyo ni muhimu kuelewa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, kuwa na maadili na uadilifu kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo Elekezi kwa watumishi wapya wa NIRC walioajiriwa na Serikali hivi karibuni Mndolwa amesema mafanikio ya Tume yanategemea mshikamano, weledi na utendaji bora wa kila mmoja kwa kuzingatia maadili na uadilifu. Amefafanua kuwa kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa kazi yake ni sehemu ya mchango mkubwa unaolenga kuboresha kilimo nchini kupitia miradi ya umwagiliaji.

“Tunaposhirikiana na kutumia ujuzi wetu kwa ubora, tunachangia moja kwa moja maendeleo ya kilimo na na kuleta tija kwa taifa. Kila mtumishi hapa ana nafasi ya kipekee na jukumu lake linategemea wengine wote,”amesema. Ameongeza kuwa “Siyo tu tunafanya kazi kwa ajira yetu, bali tunajenga historia ya maendeleo ya Taifa,” amesema Bw. Mndolwa.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *