Kundi la nchi saba, ikiwa ni pamoja na Marekani, limeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano kuimarisha kikosi cha kimataifa kilichopewa jukumu la kupambana na ghasia za magenge nchini Haiti, kulingana na barua iliyoonekana na shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Barua hiyo pia inatangaza kuundwa kwa “kundi la washirika” kusimamia ujumbe huo, ambao uliidhinishwa awali na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2023 kusaidia mamlaka ya Haiti kudhibiti ghasia zinazoongezeka katika nchi hiyo masikini ya Caribbean.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kutumwa kwa mara ya kwanza kwa Kikosi cha Usalama cha kimataifa (MSS), kilioongozwa na Kenya hapo awali, hali nchini Haiti inaendelea kuwa mbaya, huku mji mkuu, Port-au-Prince, ukiwa karibu kabisa chini y udhibiti wa magenge.

“Kikoi cha MSS hakina rasilimali na uwezo wa kushughulikia kikamilifu changamoto inayokua,” inasema barua hiyo, iliyotiwa saini na Marekani, Canada, El Salvador, Guatemala, Jamaica, Kenya, na Bahamas.

Kati ya maafisa wa polisi 2,500 ambao Misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kuimarisha Utulivu nchini Haiti ilitarajia kupeleka Haiti, ni takriban 1,000 tu kutoka nchi sita wametumwa, wakiwemo zaidi ya 700 kutoka Kenya.

“Ni kikosi kilichoimarishwa tu, kinachotolewa na ofisi ya usaidizi ya Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kuendesha operesheni za kukabiliana na magenge… kinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa udhibiti wa magenge,” inaendelea barua hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwezi Februari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipendekeza kuundwa kwa ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa kusaidia ujumbe huo, ambao pia unakabiliwa na ukosefu wa msaada wa kifedha na vifaa.

Guterres pia alipendekeza kuundwa kwa “Kundi la Kudumu la Washirika,” ambalo nchi zilizotia saini barua hiyo zilikubali kuanzisha, pamoja na Kenya ikiwa “Kamanda wa Kikosi” wa sasa.

Kundi hili litakuwa na jukumu la kupata ufadhili kwa wafanyakazi ambao haujatolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya baadaye, pamoja na kuajiri vikosi vya usalama zaidi ili kushiriki katika misheni na kuhakikisha “uwakilishi wa kimkakati na uratibu wa kikosi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *