
Wakati wa ziara yake mjini Paris siku ya Jumatano, Agosti 27, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amekutana na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Élysée. Amekubaliana naye juu ya haja ya “kufufua” na “kuimarisha” uhusiano kati ya Ufaransa na Senegal. Kisha akashiriki katika vikao vya wajasiriamali wa Ufaransa, ambapo ametaka kuwashawishi viongozi wa biashara wa Ufaransa kuwekeza tena katika nchi yake.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika ziara rasmi nchini Ufaransa, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye alipokelewa na Emmanuel Macron asubuhi ya Jumatano, Agosti 27, kwenye Ikulu ya Élysée, ambapo Dakar na Paris walielezea nia yao ya “kufufua” na “kuimarisha” uhusiano wao. Wakati Rais wa Senegal alielezea mapokezi ya mwenzake kama “mazuri,” mkuu wa nchi wa Ufaransa ameelezea kwa upande wake kama “mazungumzo bora.”
Mazungumzo haya ya kirafiki yanakuja wakati, tangu mabadiliko ya kisiasa nchini Senegal, serikali ya sasa imeendelea kudai uhuru wake kutoka kwa Ufaransa. Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, nchi hizo mbili zimekuwa zikipitia upya jalada lao la ushirikiano, ambalo hivi karibuni linatwezesha kufanyika kwa semina baina ya serikali. Lengo la mbinu hii, kulingana na Ikulu ya Élysée, ni “kuhakikisha kwamba mipango ya ushirikiano inayofanywa inawiana na vipaumbele vya serikali mpya ya Senegal.”
Wakati wa mkutano huo, majadiliano pia yalilenga usalama wa kikanda, uchumi, na maswala ya kumbukumbu, haswa mauaji ya Thiaroye.
Kuhusu suala la kwanza, marais hao wawili walizungumzia tishio la ugaidi linaloyakabili baadhi ya mataifa jirani ya Senegal, pamoja na ukosefu wa “matarajio ya mpito wa kisiasa” katika nchi kadhaa za Sahel, kwa kurejelea maneno ya ofisi ya rais wa Ufaransa.
Kuhusu suala la pili, Emmanuel Macron ametbainisha kuunga mkono mazungumzo yanayoendelea kati ya Dakar na IMF, ambayo anayaona kuwa muhimu katika kufufua uchumi wa nchi na kurejesha imani kwa jumuiya ya wafanyabiashara, ikizingatiwa kwamba Senegal inakabiliwa na madeni makubwa na imejitolea kupunguza nakisi yake ya umma. uungwaji huu mkono unakuja licha ya malimbikizo ya malipo kwa baadhi ya makampuni ya Ufaransa, hasa Eiffage, ambayo inadai euro Milioni 150 kutoka Senegal kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kikanda itakayotumiwa na treni za mwendo kasi.
Hatimaye, kuhusu sula la tatu, ingawa Emmanuel Macron sasa amekubali mauaji ya Desemba 1, 1944, kwa niaba ya Ufaransa, kiza bado kinatanda kwenye suala hilo, hasa kuhusu idadi ya vifo. Kuhakikisha kwamba Dakar na Paris zilikubali kufanya utafiti zaidi wa kihistoria ili “kupata ujuzi sahihi zaidi iwezekanavyo” wa mauaji hayo – na hasa idadi ya wahasiriwa – Ikulu ya Élysée imeonyesha kuwa misheni mpya ya wanahistoria inaweza kuja na kufanya kazi katika kumbukumbu za Ufaransa.
“Senegal inasalia kuwa nchi iliyo wazi kwa ushirikiano wowote” ambamo “una nafasi “
Kufuatia mkutano huu, Bassirou Diomaye Faye alihudhuria vikao vya wajasiriamali wa Ufaransa mchana, ambapo alikuwa mgeni rasmi. Tukio hilo lililofanyika mwaka huu katika uwanja wa Roland-Garros mjini Paris, lilimpa fursa ya kuhutubia makampuni ya Ufaransa wakati ambapo uwekezaji kutoka Ufaransa unapungua nchini Senegal, na kushuka kutoka 60% hadi 15% tu ya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.