
Watu wasiopunguwa wanane wameuawa na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa mjini Kyiv, Ukraine, usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi. Urusi imerusha ndege zisizo na rubani 629 na makombora katika shambulio “kubwa” la usiku dhidi ya Ukraine, kulingana na jeshi la Ukraine. Kyiv inasubiri “majibu” kutoka kwa ulimwengu mzima, Rais Zelensky amejibu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ilikuwa usiku mwingine wa hofu kwa mamilioni ya wakaazi wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, anaripoti mwandishi wetu wa Kyiv, Emmanuelle Chaze. Shambulio hili la hivi punde limejumuisha mashambulio ya ndege zisizo na rubani na makombora zaidi ya kumi yaliyorushwa wakati wa usiku. Urusi imerusha ndege zisizo na rubani na makombora 629 wakati wa shambulio hili, kulingana na jeshi la Ukraine.
“Shambulio lingine kubwa katika miji yetu. Mauaji zaidi,” amejibu Rais Zelensky. Mashambulizi haya yanaonyesha kuwa Urusi “inapendelea makombora ya balestiki” kuliko mazungumzo ya kidiplomasia ili kumaliza vita, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo Alhamisi asubuhi. “Urusi inapendelea kuendelea kuua badala ya kumaliza vita,” ambayo ilianza baada ya mashambuliei ya Urusi mwezi Februari 2022. Ukraine inatarajia “majibu” kutoka kwa ulimwengu, ikiwa ni pamoja na vikwazo vipya, ameongeza, hasa wito kwa China, mshirika wa Urusi, na Hungary, mwanachama wa EU, kuchukua misimamo imara.
Milipuko ya kwanza ilisikika hata kabla ya tahadhari za anga, kulingana na mashahidi kadhaa, ikimaanisha kuwa sio wakaazi wote wa Kyiv walipata muda wa kukimbilia maeneo salama. Usiku huo ulikuwa nna milipuko katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu. Zaidi ya maeneo 20 yaliathiriwa, ikiwa ni pamoja na majengo mengi ya makazi, ofisi, shule ya chekechea—ambayo iliteketezwa na miale ya moto—na miundo ya reli. Baadhi ya waokoaji 500 na zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi wanapekua vifusi, kutafuta manusura waliokwama.
Kwingineko nchini, sekta ya nishati imeathirika, na kusababisha watu 60,000 kukosa umeme, hasa katika eneo la Vinnytsia.