Chanzo cha picha, Getty Images
Kobbie Mainoo ameiambia Manchester United anataka kuondoka kwa mkopo kutafuta nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini klabu hiyo inamtaka kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 20 abaki na apiganie nafasi yake. (Athletic)
Wolves wako tayari kukataa ofa ya tatu ya Newcastle ya pauni £60m kwa ajili ya Jorgen Strand Larsen na bado wanasisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 25 hatauzwa katika dirisha hili la usajili. (Telegraph)
Tottenham wako karibu kukubaliana juu ya mkataba wa takriban pauni £60m na RB Leipzig kwa kiungo mshambuliaji wa Uholanzi, Xavi Simons, 22, baada ya kujitahidi kupunguza tishio la Chelsea kuharibu mpango wao. (Telegraph)
Baada ya kukubaliana ada kwa winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, 21, Chelsea pia wako tayari kutoa ofa ya pauni £60m kwa Simons wa Leipzig. (Metro)
Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wamefanya mawasiliano na Manchester City kuhusu uhamisho wa beki wa Uholanzi, Nathan Ake, 30. (Givemesport)
Aston Villa wako karibu kumsajili mshambuliaji Marco Asensio kwa mkataba wa kudumu kutoka Paris St-Germain baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 29 kufanya vyema wakati alipokuwa kwa mkopo Villa Park msimu uliopita. (L’Equipe)
Baada ya kumpoteza Romelu Lukaku kwa jeraha, mabingwa wa Italia Napoli wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, 22, kwa mkopo, na tayari wamefikia makubaliano ya mdomo kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark. (Gianluca DiMarzio)
Beki wa kushoto wa Manchester United na Uholanzi, Tyrell Malacia, 26, anatarajiwa kujiunga na Elche kwa mkopo wa msimu mzima baada ya kuchagua timu hiyo ya La Liga badala ya Lille. (Voetbal International)
Klabu iliyopanda daraja Serie A, Cremonese, ina nia ya kumsajili Jamie Vardy, 38, mshambuliaji wa zamani wa England ambaye amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Leicester City mwishoni mwa msimu uliopita. (Times)
Chanzo cha picha, Getty Images
N’Golo Kante, 34, ambaye alikuwa mchezaji mwenzake wa Vardy huko Leicester na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, anatarajiwa kurejea Ulaya baada ya kiungo huyo wa zamani wa Chelsea kumendewa na vilabu vya AS Monaco na Paris FC na mabingwa wa Ligi Kuu ya Saudi, Al-Ittihad. (L’Equipe )
Crystal Palace wanajiandaa kumpoteza nahodha wao Marc Guehi, 25, kwenda Liverpool, wanataka pauni £45m kwa beki huyo wa England. (Express)
Burnley wana nia ya kumsajili Florentino Luis wa Benfica, 26, lakini Marseille na Roma pia wameonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa ulinzi wa Ureno msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Rangers wamefanya mawasiliano na Everton kuhusu mpango wa mkopo kwa mshambuliaji wa Ureno, Youssef Chermiti, 21. (Sky Sports)
Beki wa Ufaransa wa Paris FC, Dimitri Colau, 19, atafanyiwa vipimo vya afya West Ham siku ya Jumamosi kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne na the Hammers. (Footmercato)