Wakfu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini wa Thabo Mbeki, unaandaa kongamano la kujadili namna ya kupata amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kongamano hilo litafanyika jijini Johannesburg, kati ya Septemba tarehe tatu hadi sita, unaolenga kutoa fursa kwa makundi mbalimbali nchini DRC kujadiliana kuhusu amani ya nchi yao.

Jarida la Jeune Afrique, limeripoti kuwa baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na changamoto zinazoikabili Jumuiya ya SADC katika harakati za kusaidia kupata amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Miongoni mwa wajumbe wanaotarajiwa kushiriki kwenye majadiliano hayo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO Donatien Nshole, wakiwemo wanasiasa rais wa zamani Joseph Kabila, Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine.

Hata hivyo, serikali ya Kinshasa kupitia msemaji wake, Patrick Muyaya imesema kongamano hilo halina manufaa na wawakilishi wa upande wa serikali wakiongozwa na Spika wa bunge Vital Kamerhe, waliokuwa wamealikwa, hawatohudhuria.

Serikali ya DRC inaonekana kupendelea mchakato wa Doha na mkataba wa Washington DC licha ya kuendelea kupata shinikizo za kuandaa mazungumzo ya kitaifa na makundi yote ili kupata mwafaka wa kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *