.

Chanzo cha picha, Reuters

Maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya takriban watu
1,000 katika milima ya Marra magharibi mwa Sudan, kulingana na kundi la waasi
la Sudan Liberation Movement/Army.

Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi siku ya
Jumapili, huku aliyenusurika akiwa mtu mmoja tu wakati sehemu nyingi za kijiji
cha Tarasin zikishuhudia “maafa” makubwa, kundi hilo lilisema katika
taarifa.

Kundi hilo limeomba
msaada wa kibinadamu kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya
kikanda na kimataifa.

Wakazi wengi
katika jimbo la Darfur Kaskazini walikuwa wametafuta hifadhi katika eneo la
Milima ya Marra, baada ya vita kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid
Support Forces (RSF) kuwalazimisha kuondoka makwao.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *