Paris, Ufaransa. Zinedine Zidane amefunguka na kubainisha kwamba sasa yupo tayari kurudi mzigoni.

Kiungo wa zamani wa boli, Zidane, 53, amejiweka kando kwenye kazi yake ya ukocha kwa kipindi cha miaka minne sasa.

Na mara kadhaa jina lake limekuwa likitajwa kuhusishwa na Manchester United hata sasa ikidaiwa kwamba anaweza kukabidhiwa mikoba endapo Ruben Amorim atafutwa kazi.

Kipindi chake cha pili cha ukocha Real Madrid kilimalizika 2021 na kumekuwa na hofu kwamba Zidane baada ya kuwa nje ya kazi hiyo ya ukocha kwa muda mrefu, anaweza asirudi tena.

ZIDA 01

Jambo hilo lingekuwa tatizo kubwa kwa kocha aliyewahi kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mfululizo na tangu alipoondoka Real Madrid hajawahi kufanya kazi kwingine.

Jumapili iliyopita, Zidane alizima uvumi wa kwamba harudi tena mzigoni, aliposema: “Nitarejea.”

Hata hivyo, Zidane anafikiria zaidi kibarua cha kwenda kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa.

Alipoulizwa kuhusu kurudi Juventus, Zidane amesema: “Sifahamu. Ilishindwa kutokea huko nyuma, nilifanya uchaguzi mwingine. Juve siku zote imekuwa kwenye moyo wangu, walinipa vitu vingi sana nilipokuja hapa kwa mara ya kwanza. Lakini, ngoja tuone.”

ZIDA 02

Ufaransa imekuwa na makocha watatu tu katika kipindi cha miongo miwili iliyopita na Didier Deschamps amekuwa akiitoa timu hiyo kwa miaka 13 mfululizo, akiwapa taji la Kombe la Dunia na Nations League.

Zidane anahesabika kama mmoja wa wachezaji mahiri kabisa wa Ufaransa, akifunga mabao 31 katika mechi 108 za kimataifa alizochezea timu hiyo kabla ya kustaafu mwaka 2006.

Mechi yake ya mwisho alishuhudiwa Zidane akimrukia kichwa Marco Materazzi kwenye kifua katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2006, ambapo Ufaransa ilipoteza mbele ya Italia kwa mikwaju ya penalti huko Ujerumani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *