Maandamano makubwa yamefanyika nchini Malaysia kuunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani himaya ya Marekani kwa Israel na jinai za utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano hayo yaliyofanyika jana baada ya Swala ya Ijumaa yamelaani vikali mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza kwa msaada na himaya ya Marekani.

Wakiwa wamebeba bendera za Palestina waandamanaji hao walisikika wakipiga nara dhidi ya Marekani na utawala ghasibu wa Israel.

 Maandamano hayo yaliishia mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Kuala Lumpur ambapo sauti za nara dhidi ya Marekanii na Iisrael zilisikika.

Waandamanaji hao, walisika wakipaza sauti “Kifo kwa Marekani, Kifo kwa Trump, Kifo kwa Israel na Palestina lazima ikombolewe,”. Aidha walilaani tabia ya Donald Trump ya kujionyesha ya kuanzisha kile kinachoitwa amani huko Gaza.

Waislamu hao walitoa wito wa kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.

Maandamano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel yamekuwa yakishuhudiwa katika kila kona ya dunia na kuonyesha jinsi walimwengu wanavyouchukia utawala huo.

Maandamano hayo yanakwenda sambamba na kuongeza himaya na uungaji mkono wa walimwengu kwa wananchi madhulumu wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza ambao kwa zaidi ya miaka miwili sasa wanakabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala huuo ghasibu.

Wikki iliyopita makumi ya miji na mikoa kote ya Uhispania ilishuhudia maandamano makubwa na migomo ya umma ya mshikamano na watu wa Gaza .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *